Mafunzo ya wafanyakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino kuhusu Sheria za Ardhi.

Kazi ya nyongeza ambayo LECIDE imefanya mwaka 2018 ni kutoa mafunzo kwa wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino kuhusu Sheria ya Ardhi Na 4 ya 1999 na jinsi ya kutatua migogoro ya ardhi katika eneo la kata ya Bwigiri.
Wafanyakazi wa wilaya wamesababisha mizozo mingi kwa kugawa ardhi bila malipo ya fidia kwa wamiliki wa ardhi wa awali.
Matokeo ya mafunzo hayo kutokana na taarifa ya Mheshimiwa Kenneth Yindi diwani wa kata ya Bwigiri yamesaidia kuokoa zaidi ya shilingi milioni 300 kutoka kwa maafisa wa ardhi ambao walitaka kuiba fedha za mali ya Halmashauri ya wilaya ya Chamwino.
Kazi zingine zitakazofanywa ni pamoja na kuwasiliana na mitandao ya NGOs nyingine za hapa nchini na za kiamataifa kwa ajili ya upatikanaji fedha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *