Portfolio

SHUGHULI ZILIZOTEKELEZWA NA LECIDE KATIKA KIPINDI CHA JANUARI 2015 MPAKA DESEMBA 2017

 • Malengo ya LECIDE kwa Mwaka 2015/2016
  Katika Mwaka 2016 LECIDE ilikuwa na malengo yafuatayo:
  a) Kuandaa mipango ya matumizi bora ya ardhi ya vijiji 15 katika Mikoa ya Iringa, Ruvuma, Njombe, Morogoro, Lindi na Mtwara.
  b) Kutoa mafunzo kwa halmashauri za Wilaya kuhusu sheria za ardhi na mbinu shirikishi za utayarishaji wa mipango ya matumizi ya ardhi.
  c) Kusaidia kupatikana kwa ardhi kwa ajili ya utekelezaji wa kilimo kwanza.
  d) Kufanya utafiti katika masuala yanayohusiana na masuala ya ardhi hasa katika maeneo yenye migogoro, uhamiaji mijini kutoka vijijini, ushirikishwaji wananchi katika kuendeleza ardhi mijini, viwango vya matumizi ya ardhi mijini na vijijini n.k
  e) Kufanya urasimishaji ardhi kwa wananchi wa Jijiji la Dar es Salaam hasa kwa wilaya ya Kinondoni.

 • UTAFUTAJI FEDHA ZA UTEKELEZAJI MIRADI YA LECIDE MWAKA 2016
  Katika mwaka wa 2016 LECIDE ilijipanga kutafuta fedha kupitia matangazo ya miradi mbalimbali.
  Mwezi Agosti 2016 lilitolewa tangazo katika gazeti la Daily News likitaka Kampuni au NGO inayoweza kuandaa mipango ya matumizi ya ardhi katika mikoa ya kanda za juu kusini kuandaa andiko la kuomba kazi hiyo.
  Madhuni ya mipango ya matumizi ya ardhi ni kupata maeneo ya kupanda miti kibiashara.
  LECIDE iliandaa andiko ambalo lilikubaliwa na kupewa kazi ya kuandaa vijiji 15 katika wilaya za Makete, Ludewa, Njombe, Songea (Madaba) na Nyasa.
  Jumla ya gharama ni shs. 293,400,000/=.

 • UTEKELEZAJI WA KUANDAA MIPANGO YA MATUMIZI YA ARDHI YA VIJIJI 15 KATIKA WILAYA ZA SONGEA (MADABA), MAKETE, NJOMBE, LUDEWA NA NYASA.
  1. Utayarishaji wa Mipango ya Matumizi ya Ardhi ya Vijiji 3 Wilaya Songea (Madaba).
  Vijiji vya kwanza kuandaa mipango ya matumizi ya ardhi ni katika wilaya ya Songea katika Halmashauri ya wilaya ya Madaba navyo ni Ifinga, Mkokngotema na Wino.
  Kazi hiyo ilianza kutekelezwa na LECIDE kwa kutumia fedha zake kwani hadi kazi za uwandani inakamilika Panda Miti Kibiashara (PFP) walikuwa hawajatoa hata sentí tano.
  Katika zoezi hili LECIDE ilipata zaidi ya hekta 29,000 za kupanda miti kibiashara.Mipango ya matumizi ya ardhi ya vijiji 3ilikamilika mwezi wa tisa na kuwasilishwa kwa Halmashauri ya wilaya ya Madaba na Programu ya Panda Miti Kibiashara mwezi huo huo wa tisa.
  Hatua ya kwanza ya uandaaji mipango ya matumizi ya ardhi ilikuwa kutoa elimun ya sheria za ardhi, mali asili na mazingira kwa Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Madaba Timu ya Halimashauri iliundwa ambayo ilitakiwa kushirikiana na wataalamu wa LECIDE kwenda vijijini kuandaa mipango ya matumizi ya ardhi.
  Hatua ya pili ilikuwa ni kutoa elimu ya sheria za ardhi, mali asili na mazingira kwa serikali za vijiji na baadaye kwa wanacnchi wote. Serikali za vijiji ziliunda timu ya kijiji ya kuandaa mipango ya matumizi ya ardhi kushirikiana na wataalamu wa LECIDE na wataalamu wa wilaya.Timu ya kijiji ilikuwa na wanawake wanne na wanaume wanne.
  Hatua ya tatu ni timu ya kijiji, wilaya na LECIDE kuandaa mipango ya matumizi ya ardhi kwa siku kumi na nne.
  Kazi hiyo ilihusu kukusanya takwimu, kuandaa ramani na kuhoji wananchi na viongozi wa kijiji kuhusu masuala ya ardhi, mali asili na mazingira, kilimo mifugo, afya, uchumi, miundo mbinu na maji.
  Mapendekezo ya mpango wa matumizi ya ardhi kwa kila kijiji yaliandaliwa.
  Hatua ya nne mipango ya matumizi ya ardhi iliwasilishwa kwa serikali ya kijiji na wananchi wote na kujadiliwa na baadaye kukubaliwa au kubadilishwa kulingana na maoni ya viongozi na wananchi.
  Hatua ya tano ripoti iliandaliwa na kuwasilishwa kwa Halmashauri ya wilaya na kuidhinishwa au kubadilishwa kulingana na maoni ya madiwani, viongozi wa wilaya na wataalamu mbalimbali.
  Baada ya kuidhinishwa iliwasilishwa Panda Miti Kibiashara (PFP) na Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi na Mkoani.
  Kazi hii ilikamilika mwezi Oktoba 2016.

  2. Utayarishaji wa Mipango ya Matumizi ya Ardhi ya Vijiji 12 katika Wilaya za Njombe, Ludewa, Makete, Songea (Madaba) na Nyasa.
  Baada ya kukamilika zoezi la vijiji vitatu vya Madaba, LECIDE iliendelea na kuandaa vijiji 12 vya wilaya zilizo tajwa kwa kufuata hatua hizo juu.Kazi hii ilianza Mwezi Oktoba 2016 na kukamilka mwezi Novemba 2016. Kazi ya vijiji vyote 15 ziliandaliwa ripoti ambazo zilipitishwa kwa kibali katika Halmashauri zote za Wilaya husika. Mgao wa ripoti zilizo idhinishwa na Halmashauri za Wilaya ulikuwa kama ifuatavyo: kila kijiji husika nakala moja, Halmashauri ya Wilaya nakala moja, Panda Miti Kibiashara nakala moja, LECIDE nakala moja na Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi nakala moja.
JEDWALI LA VIJIJI VILIVYOANDALIWA MIPANGO YA MATUMIZI YA ARDHI NA LECIDE MWAKA 2016/2017
Na. Mkoa Wilaya Vijiji Idadi
1. Njombe Njombe Lilombwi na Liwengi 2
Ludewa Maholongwa na Njelela 2
Makete Masisiwe 1
2 Ruvuma Nyasa Mkali A, Lipingo, Nkalachi, Liuli na Mango 5
Songea (Madaba) Ifinga, Mawese, Lilondo, Mkongotema na Wino 5
JUMLA 15


3. Kuweka mabango na kutoa elimu ya Hati Miliki za Kimila.

Katika mwaka 2017, LECIDE iliweka mabango katika vijiji vyote baada ya Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi kukubali ripoti zote za mipango ya matumizi ya ardhi ya vijiji 15.
Mabango huwekwa kuonyesha kila tumizi la ardhi lilipo na hiyo hutafsiri ramani ya mpango juu ya ardhi ya kijiji.
Kazi hii hufanywa na timu ileile iliyoandaa mpango na kushirikiana na wnanchi. Mabango husaidia kutenganisha matumizi ya ardhi na kuzuia mwingiliano hivyo kuondoa migogoro ya ardhi. Kazi ya pili ilikuwa kutoa elimu ya kutayarisha Hati Miliki ya Kimila kwa vijiji vyote vyenye mipango ya matumizi ya ardhi. Mabango huonyesha matumizi ya ardhi yaliyopo kijijini. Kazi hiyo husaidia kutayarisha hati miliki za kimila kwa kila tumizi la ardhi kwa wamiliki. Eneo la kilimo hutolewa hati miliki za kimila za mashamba kwa kila mwanakijiji kulingana na eneo analo kalia. Kazi kubwa inakuwa mi kuhakiki mipaka ya kila shamba au nyumba ili kuondoa migogoro baina ya wamiliki jirani. Timu ya maumizi ya ardhi hugeuzwa kuwa kamati ya kuhakiki mipaka ya mashamba na ramani huchorwa kulingana na makubaliano na majirani. Ramani hiyon huunganishwa na kuonyeshwa shamba la mmiliki na kutolewa hati miliki ya kimila. Hati miliki za kimila hazikutolewa kwa kuwa Panda Miti Kibiashara hawakuweza kuwajengea vijiji masijala za ardhi za wilaya na vijiji. Hati miliki ya kimila hutolewa katika vijiji vyenye masijala ya ardhi na wilaya. Pamoja na kutoa elimu LECIDE iliacha katika kila kijiji mifano ya hati miliki za kimila kusudi kama kijiji kikijenga masjala ya ardhi na kununua muhuri wa moto, afisa mtendaji na mwenyekiti wa kijiji wanaweza kutoa hati miliki za kimila kwa wananchi wake.JEDWALI LA VIJIJI VILIVYOANDALIWA MIPANGO YA MATUMIZI YA ARDHI NA LECIDE HALI YA UTEKELEZAJI
SNJina la KijijiWilayaMuundajiTarehe ya Kazi kukamilikaUwasilishaji Wilayani/PFPImewasilishwa NLUPCUwasilishaji Wizara ya Sheria ili kutangazwaTarehe ya Kutangazwa katika Gazeti la Serikali
1.IfingaMadabaLECIDE11.10.2016NdiyoNdiyoNdiyoBado
2.MkongotemaMadabaLECIDE12.10.2016NdiyoNdiyoNdiyoBado
3.WinoMadabaLECIDE12.10.2016NdiyoNdiyoNdiyoBado
4.LilombwiNjombe MjiLECIDE9.11.2016
5.MaholongwaLudewaLECIDE11.11.2016
6.NjelelaLudewaLECIDE9.11.2016
7.LilondoMadabaLECIDE28.11.2016
8.LiuliNyasaLECIDE24.11.2016
9.LiwengiNjombe MjiLECIDE9.11.2016
10.LipingoNyasaLECIDE3.12.2016
11.Mkali ANyasaLECIDE24.11.2016
12.NkalachiNyasaLECIDE24.11.2016
13.MangoNyasaLECIDE1.12.2016
14.MawesoMadabaLECIDE1.12.2016
15.MasisiweMaketeLECIDE12.12.20163. MATOKEO

Matokeo makubwa katika kuandaa mipango ya matumizi ya ardhi ya vijiji 15 ni upatikanaji wa ardhi kwa ajili ya Kilimo, Mifugo, Panda Miti Kibiashara, Hifadhi ya Wanyama Pori Jamii na Misitu. Katika kila kijiji kulitengwa ardhi kwa ajili ya kilimo cha mashamba madogo. Mashamba makubwa ya uwekezaji yalipatikana katika vijiji vyenye wakazi wachache na kuna maeneo makubwa.
Maeneo ya mifugo yalitengwa kulingana na upatikanaji wa ardhi na kama kijiji ni cha wafugaji.
Maeneo ya upandaji miti kibiashara yaligawanyika katika sehemu mbili kama ifuatavyo.
Vijiji katika wilaya za Madaba, Njombe, Ludewa na Makete kila kijiji kilitenga maeneno ya kupanda miti kibiashara kwa ajili ya mbao laini za mipaini na milingoti.
Vijiji vyote vya wilaya ya Nyasa vilitenga maeneo kwa ajili ya kupanda miti kibiashara ya mitiki.
Hii ni miti aghali sana na ina soko kubwa ulimwenguni.
Kila kijiji kilitenga maeneo kwa ajili ya hifadhi ya misitu ya asili. Hifadhi ya wanyama pori ilitengwa kaika vijiji vya wilaya ya Madaba. Hifadhi ya ziwani kwa mazalio ya samaki zilitengwa katika vijiji vya wilaya ya Nyasa vinavyo pakana na ziwa.
4. KAZI NYINGINE ZILIZOTEKELEZWA NA LECIDE

Kazi zingine zilizotekelezwa na LECIDE ni pamoja na:

 • Kufanya ukaguzi wa hesabu za matumizi ya fedha na vifaa vya LECIDE kwa mwaka 2016 na 2017.
 • Kushiriki katika kuandaa mpango wa Bonde la Msimbazi chini ya Benki ya Dunia.
 • Kuandaa mipango na urasimishaji ardhi Mbweni na Boko.
 • Kutoa elimu ya sheria za ardhi, mali asili , mazingira na nyinginezo zinahusiana na ardhi.
 • Kushiriki katika mikutano ya kitaalamu ya upangaji, upimaji, mazingira na uendelezaaji ardhi.
5. MATATIZO YA UTEKELEZAJI

Katika utekelezaji wa kazi LECIDE imekumbana na matatizo yafuatayo:

 • Kuchelewa kupatikana kwa fedha na fedha iliyotolewa kuwa kidogo kuliko makubaliano ya mikataba na hivyo kuchelewesha kufikia malengo kwa haraka. Mathalani, LECIDE ilikubaliana na Panda Miti Kibiashara kulipwa shs. 293,400,000/= kwa kazi ya kupanga matumizi ya ardhi na kutoa hati miliki za kimila. Lakini ghafla Mradi uliamua kutojenga masjala za ardhi za vijiji na wilaya. Kwa hiyo LECIDE imekoseshwa shs. 60,000,000/=.
 • Mashirika madogo kama LECIDE linakumbwa na tatizo la kuto ajiri watumishi muhimu wa kudumu kama mhasibu mwenye weledi wa kutosha, mtendaji mkuu na karani wa ofisi, sababu ya ufinyu wa rasilimali fedha. Sehemu kubwa ya kazi hizo hutegema kufanywa na watumishi wa kujitolea.
 • Ushiriki mdogo wa Halmashauri za Wilaya kwa kutotenga bajeti na kutoajiri wataalamu wa ardhi kunapunguza kasi ya kutekeleza shughuli za mipango ya matumizi ya ardhi.
 • Bado kuna tatizo la utoaji elimu kuhusiana na Sheria za Ardhí kwa wananchi. Juhudi lazima zifanyike katika kuwaelimisha wananchi sheria na masuala ya ardhi.
 • Wataalamu wengi wa ardhi wanakosa ufahamu wa taratibu za urasimishaji na hivyo huanzisha migogoro mingi ya ardhi mijini.  • 6. HITIMISHO NA MATARAJIO YA LECIDE

   LECIDE inakusudia kuendelea kuelekeza nguvu zake katika kutekeleza sera muhimu za kitaifa hususan Sera ya VIWANDA, KILIMO, MATOKEO MAKUBWA SASA (Big Results Now), Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025, Mkakati wa kuondoa Umasikini (MKUKUTA II), Mkakati wa Kilimo na Mifugo na Mkakati wa Taifa wa Maendeleo Vijijini, Programu ya Misitu Shirikishi, Panda Miti Kibiashara, Hifadhi ya Wanyama Pori Jamii, Hifadhi ya Pwani na Bahari, Uwekezaji katika Mashamba makubwa, Utalii na Hifadhi ya Vyanzo vya Maji, Sera ya Makazi Bora na Urasimishaji makazi na miji. Kwa kuzingatia maagizo yaliyotolewa na viongozi na será hizo muhimu, LECIDE inakusudia kutekeleza kazi zifuatazo:

   • Kutafuta fedha zaidi katika mashirika kama Shirika la kuhifadhi wanyama pori la dunia (WWF), balozi mbalimbali na idara za serikali ili kuweza kuajiri watumishi muhimu na kupanua shughuli za LECIDE
   • Kutekeleza Mipango ya Ardhi kwa kuwezesha utayarishaji mipango ya matumizi bora ya ardhi kwa ushirikishwaji katika vijiji 20 vya jirani na hifadhi za Taifa.
   • Kupanga na kupima viwanja katika mkakati wa urasimishaji katika Jiji la Dodoma, Bagamoyo, Kinondoni na halmashauri zitakazo kuwa tayari kushirikiana nasi.
   • Kutoa mafunzo kwa watendaji ngazi ya Wilaya kuhusu sheria za ardhi na mbinu shirikishi za utayarishaji wa mipango ya matumizi ya ardhi ili kuwajengea uwezo.
   • LECIDE itafanya tafiti mbalimbali kuhusu masuala ya ardhi hasa katika maeneo yenye migogoro, uhamiaji mijini kutoka vijijini, ushirikishwaji wananchi katika kuendeleza ardhi mijini, viwango vya matumizi ya ardhi mijini na vijijini n.k.

   Ripoti za Ukaguzi wa Mahesabu za miaka ya 2016 na 2017, na Majibu ya Hoja za Wakaguzi kuhusu Utawala kwa ujumla zimewasilishwa kwa msajili wa NGOs.