Kuhusu sisi

UTANGULIZI


LECIDE ni Shirika lisilo la Kiserikali lilisajiliwa tarehe 17 Julai 2015 kwa mujibu wa Sheria namba 24 ya Mwaka 2002, namba ya usajili ni OONGO/00008071.
LECIDE ni kifupisho cha Land, Environment, Community Innitiatives and Development ambayo tafsiri yake ni Ardhi, Mazingira, Jamii na Maendeleo. Shirika hili lisilo la Kiserikali limesajiliwa chini ya Idara ya Maendeleo ya Jamii katika Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Shirika limeanza kazi za kusaidia jamii mwezi Agosti 2016


DIRA YA LECIDE


Shirika imara lenye mtandao nchi nzima, na dhamira ya kuwaendeleza wananchi kiuchumi, mazingira bora na afya njema ya Watanzania wote.


LENGO KUU


LECIDE inakusudia kuwa kiongozi wa kusaidia, kuendeleza jamii kifikra na kiuchumi kwa wananchi mijini na vijijini.


MADHUMUNI YA KUANZISHA LECIDE

  1. Kuelimisha jamii ya Watanzania juu ya umuhimu wa kuhifadhi mazingira endelevu.
  2. Kuandika Makala, taarifa, mtandao na kufanya tafiti kuhusu utawala wa ardhi, mazingira, uchumi ili kubadilishana uzoefu na wadau mbalimbali.
  3. Kusaidia jamii ya kipato cha chini na kati, mijini na vijijini katika kupanga matumizi, kupima ardhi, kuandaa hati miliki, uthamini, kutatua migogoro ya ardhi na uendelezaji ardhi.
  4. Kusaidia jamii ya kipato cha chini na kati, mijini na vijijini katika kupanga matumizi, kupima ardhi, kuandaa hati miliki, uthamini, kutatua migogoro ya ardhi na uendelezaji ardhi.
  5. Kutafuta fedha toka serikalini, wahisani, na miradi binafsi ili kutekeleza malengo ya LECIDE.
  6. Kusaidia jamii ya vijijini katika mbinu za kilimo cha kisasa, ufugaji bora, upandaji miti kibiashara, kuhifadhi wanyama pori na uvuvi bora.
  7. Kutunza kumbukumbu kwa kutumia mfumo wa kisasa wa taarifa unganishi (GIS).


MAFANIKIO

Katika kipindi cha mwaka 2015 hadi 2017 LECIDE imeweza kufanikisha mipango ya matumizi ya ardhi kwa vijiji 15 chini ya Mradi wa Panda Miti Kibiashara katika wilaya za Njombe, Ludewa, Makete, Songea (Madaba) na Nyasa. LECIDE imeweza kusaidia uandaaji wa Programu endelevu ya upandaji miti katika mkoa wa Ruvuma.