Utangulizi

LECIDE ni Shirika lisilo la Kiserikali lilisajiliwa tarehe 17 Julai 2015 kwa mujibu wa Sheria namba 24 ya Mwaka 2002.
LECIDE ni kifupisho cha Land, Environment, Community Innitiatives and Development ambayo tafsiri yake ni Ardhi, Mazingira, Jamii na Maendeleo.
Shirika hili lisilo la Kiserikali limesajiliwa chini ya Idara ya Maendeleo ya Jamii katika Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Shirika limeanza kazi za kusaidia jamii mwezi Agosti 2016.

DIRA YA LECIDE
Shirika imara lenye mtandao nchi nzima, na dhamira ya kuwaendeleza wananchi kiuchumi, mazingira bora na afya njema ya Watanzania wote.

MAFANIKIO
Katika kipindi cha mwaka 2015 hadi 2017 LECIDE imeweza kufanikisha mipango ya matumizi ya ardhi kwa vijiji 15 chini ya Mradi wa Panda Miti Kibiashara katika wilaya za Njombe, Ludewa, Makete, Songea (Madaba) na Nyasa. LECIDE imeweza kusaidia uandaaji wa Programu endelevu ya upandaji miti katika mkoa wa Ruvuma

Boko – Dar es salaam, Pembeni ya barabara ya Bagamoyo, mkabala na Boko Magengeni